Tuesday, June 24, 2014

Lugha Na Maarifa

Sasa kwasababu nimejifunza kidogo lugha ya pili ya ughaibuni ... nimepata hamu ya  kujifunza lugha yangu asili ambayo sijawahi jifunza kuongea au kuelewa... na mbinu yangu ni ...kutumia  mtindo mpya wa vitabu ... teknologia ya kisasa kielimu ili utamaduni  wa kale usipotee. Tukumbuke kuwa lugha ikipotea nazo mila desturi na maarifa pia.

Hebu nijaribu kujikumbusha yale ambayo sijawahi kuyanasa...kujitahidi hata kama miaka kumi yatapita.

Kwa wale wanaopenda ufasaha na usanifu... sijahariri kikamili baada ya kuadika na pengine ngeli pia hayajaambatana lakini ujumbe nimepitisha.

Basi kitabu ni hiki hapa...sijui kama ni mtindo mzuri wa kujifunza lugha yangu lakini hakika baada ya miezi kadha nitaweza kuwaeleza kama nimefanikiwa kuhifadhi baadhi ya maneneno na sentensi mapya kwa akili na baadaye kupata kuyatamka.
Gloria Madegwa | Learn Maragoli (Teach Yourself Maragoli, Beginners Audio Book) | CD Baby Music Store

No comments:

Post a Comment