Tuesday, September 17, 2013

Kanisani na matembezi Viungani Värnamo

Leo nilitembea zaidi ya kilomita kumi...
mara yangu ya kwanza kutembea
mda mrefu hivyo
kwa zaidi ya miaka miwili

kwa mie anayependa kutembea
Ilikuwa vizuri
Kuchagua kati ya njia panda
Na kupotea

Kupata njia tena
Na Kurudi mahali ninapojua
Kujiuliza maswali mawazo yakifunguka
Kutafakari majibu yakitua


sasa... "Ninasikia kichwa, tumbo na mgongo...kifua na magoti..." maumivu yataisha


jumapili kanisani Ärken
matembezi leo viungani
Kanisani jumapili
na matembezi Viungani...
Mguu Niponye
Nyumbani Nitafika

No comments:

Post a Comment