Saturday, September 29, 2012

Kufikiria

Pumzika
Zima hisia
Acha sana kufikiria
Tulia

Ridhika
Usijisukume
Jielekeze
Uchovu isikuume

Imesemekana kwamba
Furaha sio kwa kufanya mengi
Kuridhika sio kwa kupata vyeti
Bado sijadhihirisha kama haya yote ni kweli

Kijana endelea kukazana
Tarajia
Endelea kujipea motisha
Upepo wa maisha itakufikisha

posted from Bloggeroid

No comments:

Post a Comment