Tuesday, February 2, 2010

KIMYA

Sina mengi ya kusema
Ingawa kuna mengi yametendeka
Maneno hayawezi kupangika
Kutoa maana ya yanayofanyika
Nimejitahidi kuandika
Lakini kalamu yavunjika
Sina mengi ya kusema
Ingawa kuna mengi yametendeka

Maneno mengi ningesema
Lakini sitaki kujilazimisha
Afadhali ningetenda
Na kwa vitendo mgeona
Ni vizuri ninyamaze
Na kwa kimya niwaze
Maneno mengi nigesema
Lakini sitaki kujilazimisha

Maneno hayawezi toka mdomoni
Kabla ya kamilike akilini
Kuropokwa na kukosa maana
Si vile ningependa kujulikana
Wacha kwanza mawazo kupangana
Halafu ulimi kutangaza
Maneno hayawezi toka mdomoni
Kabla ya kamilike akilini

Kuna mengi ya kuelewa
Kuna mengi ya kufikiria
Na fikira zikikoma
Basi maneno yataisha
Sijaacha kufikiriria
Sijaacha kuongea
Ni tu maneno yangu naweka akiba
Nitayaseme yote pamoja na riba


James Adolwa
February-02-2010

4 comments:

 1. Ni kweli kimya ulikuwa ,
  umesema kweli kabisa,
  kusema lazima kufikiria,
  Huwezi kuropoka tu,
  Asante kwa shairi nzuri kaka James.

  ReplyDelete
 2. Ni kweli hungependa kuropokwa,
  kwa kutapika maeno yasiyo na maana,
  ni bora uyawaze, kabla ya kutoporokwa.

  Shairi lako nzuri, sifa twalipa,
  kwa wanataifa wapokee,wasomee na kutii.

  mie naye kwangu shukran, kwa yake uwazayo.

  ReplyDelete
 3. Asante...hukuniachia jina lakini nadhani nilipata ujumbe wako kwa email...zaidi ya mwaka imepita tangu nilisome hili shairi. Asante kwa kuisoma...hakika nitawasiliana nawe hivi karibuni

  Asante

  ReplyDelete